• FAQ |
    • Staff Mail |
VETA
VETA

The United Republic of Tanzania Ministry Of Education Science And Technology Vocational Education And Training Authority Skilled Labour Force The Future Of Tanzania

  • Home
  • About Us
    • History
    • Institutional Arrangement
    • Organization Structure
  • Training Delivery
    • CBET Approach
    • Institutional Based Training
    • RPL Program
    • Dual Apprenticeship Program
    • INTEP Program
    • SEP Program
  • VET Zones
    • Dar Es Salaam Zone
    • Eastern Zone
    • Western Zone
    • Central Zone
    • South East Zone
    • South West Zone
    • Highland Zone
    • Lake Zone
  • ICT Services
    • VETMIS
    • VCRS
    • GePG
    • VIBALI KUSAFIRI NJE YA NCHI
    • IGAS
    • eVETS
    • VET REGISTERED CENTRES
    • APPLICANTS SELECTION PORTAL
    • VETA SKILLS
  • Other Website
    • Morogoro Vocational Teachers Training College
    • Kipawa ICT Centre
    • Dual Apprenticeship
  • Publications
    • VET Guidlines
    • VET Forms
    • VET Report
  • Media Center
    • Press Release
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • News

Wenye Ulemavu waiomba VETA kuhuisha mitaala yake

Posted on: Tuesday, 04 December 2018

Mratibu wa Idara ya Maendeleo Vijana na Chipukizi wa Chama cha Wasiiona Tanzania, Kiongo Itambu ameiomba Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kuhuisha mitaala yake ili iweze kuwa rafiki zaidi kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa watu wenye uelemavu wa aina zote hasa wasioona.

Itambu alisema hayo jana Novemba 29, 2018 wakati akipokea hundi ya Shilingi laki tano kutoka VETA kwa ajili ya kuwezesha kiongozi mmoja wa chama hicho kuhudhuria maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu itakayofanyika Desemba 1, 2018 mkoani Simiyu.

Alisema chama hicho kinatambua mchango wa VETA katika kuwapatia vijana ujuzi na kwamba watu wengi zaidi wenye ulemavu wakipata ujuzi huo utawasaidia kuinua uchumi wao na kuchangia pato la taifa.

“Tunaomba sana VETA iwaangalie kwa jicho la pili watu wenye ulemavu ili nao waweze kupata fursa zaidi ya kupata elimu ya ufundi stadi kwa kuandaa mitaala na mazingira rafiki ya kufundishia” Alisema

Aliishukuru VETA kwa msaada huo na kuomba Mamlaka hiyo iendelee kushirikiana nao kwa karibu katika shughuli mbalimbali wanazozifanya.

Naye Afisa Uhusiano wa VETA Dora Tesha alimsihi kiongozi huyo kutumia majukwaa mbalimbali na mikutano ya vyama vya wenye ulemavu kuwafahamisha watu hao juu ya fursa zilizopo katika vyuo vya Ufundi stadi nchini na kuwahamasisha kuzitumia vyema kupata ujuzi na kuweza kujiajiri wenyewe.

Alisema VETA imekuwa ikitoa mafunzo kwa watu wenye ulemavu ingawa idadi kubwa ya wanaojitokeza ni wenye ulemavu wa viungo ambapo kwa mwaka 2017 jumla ya vijana wenye ulemavu 334 walipata mafunzo katika fani mbalimbali katika vyuo vya ufundi stadi na kwamba kati yao 214 ni wenye ulemavu wa viungo na 11 pekee ndiyo wasiiona.

Alimuomba kiongozi huyo kuialika VETA kwenye makongamano na mikutano mbalimbali inayowakutanisha watu wenye ulemavu ili kuweza kutoa elimu juu ya fursa zilizopo katika vyuo vya Ufundi stadi na kufafanua hoja mbalimbali.


Share :

Announcements


  • Dec 04

    Majina ya waliochaguliwa kujiunga na vyuo vinavyomilikiwa na VETA

Publications


  1. 169 VACANCIES ANNOUNCEMENT - Dec 29, 2018
  2. Jinsi ya kushiriki katika Shindano la Ubunifu/Ugunduzi - Dec 28, 2018
  3. Fani na madaraja zitakatozotolewa - Sep 29, 2018

Popular News


  • VETA envisions Tanzania with sufficient and Competent artisans

    Monday, 24 September 2018
  • VETA yakabidhi vifaa vyenye thamani milioni 41 kwenye chuo cha wenye ulemavu

    Monday, 24 September 2018
  • Madereva wasio na VYETI wasio na vyeti waaswa kuchangamkia fursa za mafunzo VETA

    Wednesday, 26 September 2018
  • Mikoa ya Geita,Njombe,Rukwa na Simiyu Kupata Vyuo Vya VETA

    Wednesday, 26 September 2018
  • The VETA Hotel and Tourism Training Institute to introduce tourism courses

    Tuesday, 04 December 2018
  • VETA,CARE na SAGCOT zaingia makubaliano kuimarisha ujuzi sekta ya kilimo

    Tuesday, 04 December 2018
  • Wasichana wahamasishwa kujifunza Ufundi Stadi

    Tuesday, 04 December 2018
  • VETA kuratibu mashindano ya ubunifu wa ufundi stadi, sekta isiyo rasmi

    Tuesday, 04 December 2018
  • View All

Video

MATUKIO MBALIMBALI WAKATI WA MAONESHO YA SABASABA 2018
Video zaidi

Quick Links

  • VETMIS
  • VCRS
  • GePG
  • VIBALI VYA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • IGAS
  • eVETS
  • VET REGISTERED CENTRES
  • APPLICANTS SELECTION PORTAL
  • VETA SKILLS
  • VET APPLICATIONS

Related Links

  • Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia
  • NACTE
  • CTI
  • ATE
  • SIDO
  • Prime Ministers Office,Labour,Youth Employment and Persons with Disability

World visitors tracker

hit counter

Contact Us

    VETA HEAD OFFICE

    Address: PO BOX 2849 Dar Es Salaam

    Telphone: +255 22 2863409

    Fax: +255 22 2203156

    Barua pepe: info@veta.go.tz

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

© 2018 - VETA Head Office