The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
BRELA yatoa elimu kwa washirki wa VETA Sabasaba kuhusu miliki bunifu
Posted on: Friday, 05 July 2024
BRELA yatoa elimu kwa washirki wa VETA Sabasaba kuhusu miliki bunifu
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), leo, tarehe 4 Julai 2024, imetoa elimu kwa washiriki wa VETA kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (Sabasaba), kuhusu miliki bunifu.
Akizungumza na washiriki wa VETA kwenye maonesho hayo, Afisa usajili wa BRELA, Stanislaus Kigosi amesema kilichowasukuma kukutana na washiriki wa VETA Sabasaba ni kutokana na kutambua kwamba VETA kuna ubunifu mwingi kutokana na namna ya utoaji mafunzo ya ufundi stadi.
“Kutokana na VETA kuwa na bunifu zinazo tatua changamoto za kijamii, zinazohusu mambo ya teknolojia na ujasiriamali ndio kilicho tusukuma kuja kutoa elimu hii inayohusu ulinzi wa miliki bunifu," amesema Kigosi.
Naye Sada Rashidi (Usajili) ameshauri pia kulinda alama za biashara na rajamu (brand) za bidhaa zao.