The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
CPA Kasore: Kasimamieni utoaji mafunzo ya ufundi stadi kwa ubora
Posted on: Friday, 19 April 2024
CPA Kasore: Kasimamieni utoaji mafunzo ya ufundi stadi kwa ubora kulingana na mahitaji ya soko la Ajira
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) CPA. Anthony Kasore, amewaagiza wasimamizi wa mafunzo ya ufundi stadi kwenye vyuo vya VETA kuimarisha utoaji mafunzo ya ufundi stadi kuendana na mahitaji ya soko la ajira.
CPA. Kasore ametoa maagizo hayo wakati wa kikao kilichowakutanisha wajumbe wa Menejimenti ya VETA Makao makuu, Wakurugenzi wa Kanda na wakuu wa vyuo vya VETA kilichofanyika jijini Dodoma leo tarehe 19 Aprili, 2024.
Kasore amesema Serikali imeiamini VETA kutoa mafunzo ya ufundi stadi hapa nchini, hivyo ni wajibu wa watendaji wa VETA kutekeleza jukumu hilo kwa weledi.
“nawahimiza kwa dhati kuwa mkatimize jukumu tulilonalo la kutoa mafunzo bora kulingana na mahitaji ya soko la ajira ili tuweze kuzalisha nguvukazi ya vijana bora katika fani,” amesema
CPA Kasore ameeleza kiu yake ya kuona watumishi wa VETA wanaimarisha ubora wa mafunzo na kasi ya utoaji mafunzo ili wananchi wote wapate mafunzo hayo kwa ubora na hatimaye kuwa na nguvukazi mahiri kwa ajili ya kushiriki kwenye shughuli za kiuchumi.