Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (VETA) inawatangazia Wananchi kuwa imefungua rasmi vyuo vipya sita (6) vya Ufundi Stadi ambavyo ni Ileje (Mbeya), Nkasi (Katavi), Urambo (Tabora), Namtumbo (Ruvuma), Kanadi (Bariadi-Simiyu), Nyamidaho (Kasulu-Kigoma). Vyuo hivyo vitaanza kutoa mafunzo katika mwaka wa masomo 2020.
Fomu za kujiunga na mafunzo zitaanza kutolewa tarehe 1 Agosti hadi 15 Septemba 2019. Watu wote wanaohitaji kujiunga na mafunzo ya ufundi stadi wanakaribishwa na wanaombwa wafike katika vyuo vilivyo karibu nao kama ilivyooneshwa kwenye jedwali lifuatalo ili kuchukua na kujaza fomu za kujiunga.
VETA HEAD OFFICE,
12 VETA Road.
41104 Tambukareli,
P.O. BOX 802, Dodoma Tanzania,
Email: info@veta.go.tz
Telephone: +255 26 2963661
Fax: +255 22 2863408
Url: www.veta.go.tz
© 2018 - VETA Head Office