The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
MKATABA WA KUUNDA MABARAZA YA WAFANYAKAZI WA VETA WAHUISHWA
Posted on: Tuesday, 12 December 2023
MKATABA WA KUUNDA MABARAZA YA WAFANYAKAZI WA VETA WAHUISHWA
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) na Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu,Sayansi, Teknolojia, Habari, Ufundi Stadi na Utafiti (RAAWU)wametia saini Mkataba wa Kuunda Mabaraza ya Wafanyakazi wa VETA.
Hafla ya utiaji saini imefanyika leo tarehe 12 Desemba, 2023, katika Ofisi za VETA Makao Makuu jijini Dodoma na kushuhudiwa na viongozi wa VETA na RAAWU.
Kusainiwa kwa Mkataba huo wa miaka mitatu (2023 – 2026) kunatoa fursa ya kuanza kwa mchakato wa kuunda mabaraza ya Wafanyakazi wa VETA kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu za ushirikishwaji wa Wafanyakazi mahala pa kazi.
Katibu wa RAAWU Taifa, Ndg. Joseph Sayo, amesema RAAWU itaendelea kushirikiana na uongozi wa VETA katika kuhakikisha malengo ya VETA yanafikiwa na masuala yanayohusu wafanyakazi yanashughulikiwa kwa wakati.
Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dkt. Prosper Mgaya, amesema VETA itatimiza wajibu wake katika kutekeleza Mkataba huo na kuushukuru uongozi wa RAAWU kwa ushirikiano wanaoendelea kuutoa kwa VETA.
Mkataba wa Kuunda Mabaraza ya Wafanyakazi ulioisha muda wake ulidumu kwa miaka mitatu (2020 – 2023).