The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
MKURUGENZI TVET AHIMIZA UBUNIFU WA MATUMIZI YA TEHAMA KATIKA KUTATUA CHANGAMOTO ZA JAMII
Posted on: Wednesday, 14 May 2025
MKURUGENZI TVET AHIMIZA UBUNIFU WA MATUMIZI YA TEHAMA KATIKA KUTATUA CHANGAMOTO ZA JAMII, KUONGEZA UZALISHAJI
Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (TVET), Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Fredrick Salukele amewahimiza wakufunzi wa Chuo cha TEHAMA cha VETA Kipawa kutumia ubunifu katika TEHAMA ili kutatua changamoto za jamii na kuongea uzalishaji.
Dkt. Salukele ameyasema hayo alipotembelea katika chuo hicho, kilichopo jijini Dar es Salaam, tarehe 5 Mei, 2025.
Amesema ni vyema kuwa wabunifu ili TEHAMA itumike kwa ufanisi katika utoaji mafunzo, lakini pia katika kutatua changamoto za jamii. .
Amesema chuo hicho ni maalum kwa ajili ya mafunzo ya TEHAMA, hivyo kinategemewa kuzalisha wahitimu mahiri wenye uwezo wa kutumia ujuzi wao kurahisisha uendeshaji wa shughuli mbalimbali na kutatua changamoto zinazoikabili jamii.
“Msisitizo wangu kwenu ni kuhakikisha mnatoa mafunzo bora, mnafanya ubunifu utakaoweza kutatua changamoto zinazoikabili jamii yetu na kutoa huduma za kitaalamu kwa jamii ,” Dkt. Salukele amesema.
Dkt.Salukele amesema chuo hicho kina fursa kubwa ya kufanya uzalishaji kupitia utoaji wa huduma mbalimbali za TEHAMA kwa jamii inayowazunguka na kuwataka kufanya ubunifu na kutumia vyema fursa hizo ili kujiongezea kipato.
Amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ina mategemeo makubwa sana na VETA katika kuwawezesha wananchi kujipatia ujuzi na kuwataka wafanyakazi kutimiza wajibu wao kikamilifu ili kufanikisha azma hiyo.