The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
Timu ya Mpira wa Miguu VETA Makao Makuu jana tarehe 25 Septemba, 2024 ilkubali kufungwa kwa taabu goli moja bila na timu ya hospitali ya Benjamin Mkapa.
Mechi hiyo iliyochezwa katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), timu ya Hospitali ya Benjamin Mkapa ilifanikiwa kupenya katika ulinzi mkali wa wachezaji wat imu ya VETA Makao Makuu katika dakika ya 36 na kufanikiwa kupachika goli lilioipa ushindi.
Mashindano hayo ni muendelezo wa mechi za kirafiki zinazoendelea ikiwa ni maandalizi ya kuelekea mashindano ya Shirikisho la michezo la Mashirika ya Umma, taasisi na makampuni binafsi (SHIMUTA).
Hadi kipyenga cha dakika tisini kinapulizwa, timu ya hospitali ya Benjamin Mkapa ilipata goli moja na timu ya VETA Makao Makuu kuambulia patupu!!