The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
VETA, CMT mbioni kuingia makubaliano ya mashirikiano
Posted on: Wednesday, 14 May 2025
VETA, CMT mbioni kuingia makubaliano ya mashirikiano
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) na viongozi wa chama cha mafundi Tanzania (CMT), leo tarehe 8 Mei, 2025 wamekutana jijini Dar es Salaam kujadili namna watakavyoweza kuingia katika mashirikiano.
Lengo la kuingia mashirikiano baina ya taasisi hizi mbili ni kuongeza fursa kwa mafundi wengi zaidi kuweza kunufaika na fursa zilizopo kwenye mafunzo ya ufundi stadi hasa katika kurasimisha ujuzi wao kupitia VETA.
VETA ina programu ya urasimishaji ujuzi kwa mafundi waliopata ujuzi nje ya mfumo rasmi wa mafunzo.
VETA na CMT watashirikiana kuwapata mafundi wenye ujuzi lakini hawana vyeti, hivyo kupitia programu ya urasimishaji ujuzi mafundi hao watafanyiwa tathmini na kubaini mapangufu waliyonayo na kisha kupatiwa ujuzi na baada ya mafunzo watatunukiwa vyeti.