The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
VETA Kanda ya Kaskazini yashika Nafasi ya Tatu Katika Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kaskazini 2025
Posted on: Wednesday, 20 August 2025
VETA Kanda ya Kaskazini yashika Nafasi ya Tatu Katika Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kaskazini 2025
Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Kaskazini, Bi. Monica Mbele, akiwa ameshika cheti cha ushindi baada ya VETA kuibuka Mshindi wa Tatu katika kundi la Taasisi za Elimu kwenye Maonesho ya Nanenane kwa Kanda ya Kaskazini.
Mshindi wa kwanza katika Maonesho hayo alikuwa ni Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela na wa pili Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA).
Maonesho hayo ya 31 kwa Kanda ya Kaskazini yalifanyika kuanzia tarehe 1 hadi 8 Agosti 2025, katika viwanja vya Themi, Njiro vilivyopo jijini Arusha.
Mgeni rasmi katika maonesho hayo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Kenan Kihongosi.