The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
VETA KUTOA MAFUNZO BURE KWA KUNDI LA WANAWAKE NA SAMIA KATIKA VYUO VYAKE KOTE NCHINI
Posted on: Friday, 11 July 2025
VETA KUTOA MAFUNZO BURE KWA KUNDI LA WANAWAKE NA SAMIA KATIKA VYUO VYAKE KOTE NCHINI
Mamlaka ya Elimu na mafunzo ya Ufundi Stadi itaendelea kutoa mafunzo bure kwa Kundi la Wanawake na Samia katika vyuo vyake nchini ili kuliwezesha kundi hilo kupata stadi za kuendesha shughuli mbalimbali za kiuchumi.
Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA Anthony Kasore amesema hayo tarehe 25 Juni, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa VETA Makao Makuu alipo kutana na Mwenyekiti wa wanawake na Samia Tanzania ambae aliambatana na wenyeviti na makatibu wa wanawake na Samia ngazi ya mikoa.
CPA Kasore amesema VETA itaendelea kutoa mafunzo kwa kundi hilo la wanawake kote nchini, kama ambavyo mafunzo hayo yalivyoanza kutolewa katika chuo cha VETA Dodoma.
“Tuna wakaribisha sana VETA muendelee kuitumia fursa hii ya kupata ujuzi bure ili muweze kujikwamua kiuchumi. Tunaamini ukimuwezesha mwanamke kiuchumi basi umeisaidia jamii nzima na sisi tumelenga kuwakomboa wanawake kiuchumi,” amesema CPA Kasore.
Aidha CPA Kasore amelitaka pia kundi hilo la wanawakena Samia linalopata mafunzo katika kozi za muda mfupi katika vyuo mbalimbali na VETA kuendelea kuwakusanya wanawake wengine ambao hajawapata ujuzi na kuwaleta katika vyuo vya VETA ili kupata ujuzi, kwani jukumu kubwa la VETA ni kuhakikisha linatoa ujuzi kwa wanachi ili kujikwamua kiuchumi.
“VETA tumekuwa tukitoa mafunzo ya fani mbalimbali nyinyi kama wanawake na Samia mnaweza mkakusanya hata mabinti mkawaleta VETA wakapata mafunzo ya wafanyakazi wa majumbani au mafunzo ya kufanya usafi wa mazingira maofisini, mafunzo ya mapishi, kwani tunachohitaji sisi ni watu wapate ujuzi,” ameongeza CPA.
Akihitimisha mazungumzo yake na kundi hilo, CPA Kasore amemshukuru Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kufanya uwekezaji mkubwa VETA hasa kwa ujenzi wa vyuo unaoendelea ambapo vyuo 65 vinaendela kujengwa lakini pia uwekezaji kwenye eneo la vifaa vya vya mafunzo vya kisasa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Wanawake na Samia Tanzia na Mkoa wa Dodoma, Fatuma Madidi amemshukuru Mkurugenzi Mkuu wa VETA kwa kuridhia kundi hilo kubwa la wanake kupata mafunzo ya Ufundi stadi katika kila Mkoa hapa nchini.
“Mkurugenzi nikupongeze kwa kuweza kutupatia nafasi hii ya kupata mafunzo katika vyuo vya VETA kote nchini,vtena bure, sisi tumefarijika sana, tunaahidi kuendelea kuitumia fursa hiyo vizuri ili tuweze kujikwamua kiuchumi,”amesema.