The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
VETA KUWAJENGEA UWEZO WADHIBITI UBORA WA MAMLAKA YA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR
Posted on: Thursday, 12 September 2024
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeendaa semina ya kuwajengea uwezo Maafisa Udhibiti Ubora kutoka Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar (VTA) ili kuimarisha utendaji wao.
Akizungumza katika ufunguzi wa semina hiyo, jana, tarehe 11 Septemba 2024, Mkurugenzi wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Dkt. Abdallah Ngodu, amesema semina hiyo ni ya siku tatu, ambapo maafisa kutoka VTA watapitishwa katika miongozo mbalimbali ya udhibiti ubora na viashiria vya ubora katika utoaji na usimamizi wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi au mafunzo ya amali.
Mkaguzi Mkuu wa Vyuo na Vituo vya Mafunzo ya Amali Zanzibar (VTA), Mhandisi Ibrahim Haji, amesema Maafisa Uthibiti Ubora kutoka VTA wana lengo la kujifunza kutoka VETA namna bora ya kufanya kaguzi ili kuboresha utendaji kazi na kufanya mafunzo ya ufundi amali yabaki kwenye ubora uliokusudiwa.