The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
VETA, Vivo Energy kushirikiana kuimarisha utoaji mafunzo ya ufundi nchini.
Posted on: Wednesday, 14 May 2025
VETA, Vivo Energy kushirikiana kuimarisha utoaji mafunzo ya ufundi nchini.
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi imefanya mazungumzo na kampuni ya Vivo Enegy ya jijini Dar es Salaam, leo tarehe 9 Mei, 2025 kwa lengo la kuanzisha ushirikiano ili kuimarisha utoaji mafunzo ya ufundi stadi nchini.
Majadiliano hayo yameongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore aliyeambatana na Menejimenti ya VETA. Kwa upande wa Vivo Energy iliwakilishwa na Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Mohamed Baugriba.
Makubaliano hayo yanalenga kutoa mafunzo sahihi ya utumiaji na utunzaji wa vilainishi vya kwenye magari, kuongeza fursa za vijana (wanafunzi) na kufanya mafunzo kwa vitendo (practical training) kwenye vituo vya kuuzia mafuta (Shells na Engine).
Ushirikiano huo utawezesha vijana kupata ujuzi wa matumizi ya vilainishi hivyo kujipatia kipato na fursa kwenye mjumuiko wa biashara nzima ya Engine pamoja na Shells.
Aidha vijana hao watapata elimu sahihi ya utunzaji wa mazingira hasa kwenye maeneo ambapo vilainishi vinatumika.