The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeibuka mshindi wa kwanza kwenye kundi la Taasisi za Elimu na Vyuo vya Mafunzo nchini katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo (Nanenane), 2025.
VETA imeibuka mshindi wa kwanza mbele ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam walioshika nafasi ya pili na chuo Kikuu Ardhi iliyoshika nafasi ya tatu.
Akipokea cheti cha ushindi huo tarehe 8 Julai, 2025, Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore amewapongeza na kuwashukuru Washiriki wa Maonesho hayo kutoka vyuo mbalimbali vya VETA nchini na kuwahimiza kwenda kuendelea kutoa mafunzo ili iwe chachu kwa wananchi kuendelea kuja kujiunga na vyuo vya VETA.
"Tunaongelea Tanzania inayofanya kazi ya kuandaa watu wake kupata ujuzi wa kuweza kujiajiri, kuajiriwa na kuajiri wengine hivyo ushindi huu ukatupe hamasa ya kuendelea kuwapa ujuzi na maarifa yatakayowawezesha kutekeleza shughuli zao za kila siku kwa weledi" amesisitiza Kasore.
Maonesho ya Nanenane, 2025 yalifunguliwa rasmi tarehe 1 Julai, 2025 na Mhe.Dkt.Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kufungwa rasmi tarehe 8 Julai, 2025 na Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo aliongeza siku mbili zaidi ya kuendelea kwa Maonesho hayo ili kuwapa fursa zaidi wananchi kutembelea na kujifunza.