The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) inashiriki katika Mashindano ya 10 ya Ufundi Afrika (Africa Technical Challenge (ATC) yaliyozinduliwa, tarehe 28 Julai, 2025 nchini Kenya.
Katika Mashindano hayo Tanzania inawakilishwa na wanafunzi kutoka vyuo vya VETA Dodoma na Kipawa wakiwa wamegawanyika katika makundi mawili ya mashindano ambayo ni CNC na Uundaji wa Mifumo ya Simu (Mobile App Development).
Kundi la CNC linaundwa na wanafunzi Patrick Ezekiel Patrick, Godwin Justine Ibrahim, na Severin Leonard Francisco kutoka Chuo Cha VETA Dodoma, wakiongozwa na mwalimu Hilary Desderius Nkwera ambao wanashiriki wakiwa nchini Kenya.
Kwa upande wa kundi la Mobile App Development, wanafunzi Justin January Severine, Beatrice Mgalonje Magawa, na Daudi Azaria Daudi kutoka Chuo cha Kipawa ICT wanashiriki mashindano kwa njia ya mtandao, wakiwa Tanzania kundi huku wakiongozwa na mwalimu Ricky Sambo.
Mashindano haya yanatarajiwa kukamilika tarehe 28 Agosti 2025, ambapo washindi kutoka kila kundi watatangazwa rasmi na kutunukiwa zawadi mbalimbali kwa kutambua umahiri wao katika maeneo husika ya ujuzi.
Kupitia mashindano hayo, walimu na wanafunzi wa VETA wanapata nafasi ya kuongeza uzoefu wa kimataifa, kujifunza teknolojia za kisasa zinazotumika katika viwanda pamoja na kujenga uwezo wa kushindana katika soko la ajira la kimataifa.
Aidha, kupitia mashindano haya, VETA inapata fursa ya kuanzisha mitandao ya ushirikiano na taasisi nyingine za mafunzo na sekta binafsi ndani na nje ya Afrika, jambo linalosaidia kuimarisha mfumo wa mafunzo ya ufundi nchini.
VETA inaendelea kuwahamasisha vijana wa Kitanzania kuchangamkia fursa za mafunzo ya ufundi stadi, kwa kuwa ndiyo njia sahihi ya kuwajengea uwezo wa kujiajiri na kuajirika katika soko la ajira linalobadilika kwa kasi.