Jumla ya vijana 13,961 wa mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Mtwara wamenufaika na mafunzo ya ufundi stadi kupitia mradi wa Via Jiandalie Ajira unaotekelezwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Vijana (International Youth Foundation-IYF).
Mkurugenzi wa IYF Tanzania Joan Kimirei amesema kuwa vijana hao walipatiwa mafunzo ya ufundi stadi yaliyoenda sambamba na stadi za maisha na ujasiriamali ili kuwajengea uwezo wa kuanzisha miradi yao baada ya kuhitimu.
Kimirei amesema hayo wakati wa warsha ya kujenga ufahamu kwa wadau wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi kuhusu mradi wa Via: Jiandalie Ajira wa Shirika hilo uliofanyika mkoani morogoro tarehe 15 hadi 16 Oktoba, 2020 na kuwashirikisha Wakurugenzi wa Kanda, Wakuu wa Vyuo, Waratibu wa Mafunzo na Wakufunzi kutoka vyuo vya ufundi stadi.
Kimirei amesema pamoja na mambo mengine mradi huo, ulilenga kuwapatia vijana ujuzi na mafunzo ya ujasiriamali ili kukabiliana na tatizo la ajira.
Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dkt. Pancras Bujulu amesema kuwa mradi huo umefungua mlango wa ajira kwa vijana na kwamba VETA itaendeleza baadhi ya programme za mafunzo yaliyokuwa yakitolewa kupitia mradi, ikiwemo kutumia mtaala wa KTS (Key To Success) kwenye kozi za muda mfupi.
Mradi wa Via: Jiandalie Ajira ulianzishwa mwaka 2018 na unatarajiwa umalizika mwaka huu 2020.
VETA HEAD OFFICE,
12 VETA Road.
41104 Tambukareli,
P.O. BOX 802, Dodoma Tanzania,
Email: info@veta.go.tz
Telephone: +255 26 2963661
Fax: +255 22 2863408
Url: www.veta.go.tz
© 2018 - VETA Head Office