The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
WALIMU 50 WA VETA WAJENGEWA UWEZO WA KUTOA MAFUNZO KWA WENYE MAHITAJI MAALUM
Posted on: Friday, 11 July 2025
WALIMU 50 WA VETA WAJENGEWA UWEZO WA KUTOA MAFUNZO KWA WENYE MAHITAJI MAALUM
Jumla ya walimu 50 wa vyuo vya VETA wamejengewa uwezo na mbinu za utoaji Mafunzo sahihi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.
Mafunzo hayo ya wiki moja, yanayofanyika katika Ukumbi wa hoteli ya chuo cha Ufundi Don Bosco, jijini Dodoma yameanza tarehe 23 Juni, 2025 na yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 27 Juni, 2025.
Akizungu na washiriki wa Mafunzo hayo, Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Antony Kasore amewataka kwenda kuyatumia Mafunzo hayo kama fursa ya kuibua na kuwasaidia wanafunzi na watu wenye mahitaji maalum wanaotamani kutapa Ujuzi kupitia Mafunzo ya Ufundi stadi yanayotolewa katika vyuo vya VETA.
“Idadi ya wanafunzi wenye mahitaji maalum wanaohitaji kupata mafunzo ya Ufundi Stadi katika vyuo vyetu imekuwa ikiongezeka huku kukiwepo na idadi ndogo ya walimu wenye uwezo na mbinu stahiki za kuwapa mafunzo wanayohitaji. Nawasihi mkaitumie elimu hii kuwapa Mafunzo bora sawa na ujuzi wanaopewa wanafunzi wengine wasio na mahitaji maalum” alisisitiza Kasore.
Akimshukuru Mkurugenzi Mkuu, kwa niaba ya walimu hao, Mwalimu Fadhila Kusaga kutoka chuo cha VETA-Mtwara ameahidi kuwa watakwenda kutoa Mafunzo ya ufundi stadi bila kutazama hali ya mtu na kuwataka walimu wenzake kwenda kuwa mabalozi wa kuwahamasisha wananchi katika maeneo yao kuwaibua na kuwapeleka watu wenye mahitaji maalum kupata ujuzi utakaowawezesha kujikwamua kiuchumi.
Naye mratibu wa Mafunzo hayo, ambaye ni Afisa Mkuza Mitaala Mwandamizi kutoka VETA Makao Makuu, Bi. Happiness Salema amesema sanjari na mafunzo hayo, wameweza pia kuwa na kikao kazi cha wataalamu wa fani ya Utalii na Ukarimu kutoka VETA, Chuo cha Taifa cha Utalii na Chuo cha Wanyama pori (MWEKA) ambao kwa pamoja wanapitia na kuuhusha mitaala iliyoisha muda wake ya TG-NTA 4, 5 na 6 na kuandaa mitaala mipya ya sita ya TTO na TG ya NTA 4,5 na 6.