The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
WATUMISHI WAPYA KADA YA UNUNUZI NA UGAVI VETA WAPEWA MAFUNZO ELEKEZI
Posted on: Thursday, 15 May 2025
WATUMISHI WAPYA KADA YA UNUNUZI NA UGAVI VETA WAPEWA MAFUNZO ELEKEZI
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi kupitia Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi, tarehe 6 Mei, 2025 imetoa mafunzo elekezi ya kuwajengea uwezo watumishi wapya 33 wa kada ya Ununuzi na Ugavi.
Mafunzo hayo yamefanyika katika Chuo cha VETA Dodoma na kuongozwa na Mkuu wa Kitengo hicho Bi. Witnes Mgimba, akishirikiana na Maafisa Ununuzi wa VETA Makao Makuu.
Bi.Mgimba amewataka watumishi hao kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa kuzingatia maadili ya ununuzi na ugavi pamoja na Sheria na Kanuni za ununuzi wa umma.
“Mnapoenda kuanza kutekeleza majukumu yenu epukeni kushirikiana na watu wenye nia ovu kwenye shughuli za ununuzi kwa kuwa utakapokosea utawajibishwa kwa makosa yako ,hivyo kazingatieni sana swala la uadilifu,” amesema.
Aidha Bi. Mgimba ameishukuru Serikali kwa kuipatia VETA watumishi hao 33 wa kada hiyo kwa wakati mmoja, na amewataka watumishi hao kwenda kufanyika msaada katika vituo vyao walivyopangiwa.
Kwa upande wake Afisa Ununuzi Mwandamizi wa VETA Makao Makuu, Ndg. Christopher Msigwa, amesema mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo watumishi wapya kuhusiana na shughuli za ununuzi wa Umma, usimamizi wa vifaa na mali za Mamlaka kwa kutumia mfumo wa GAMMIS, umuhimu wa utunzaji wa kumbukumbu za ununuzi na kuzingatia maadili na miongozo ya wataalamu wa ununuzi.