The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
Waziri Mkenda asisitiza kipaumbele mafunzo ya ufundi stadi sambamba na upanuzi wa miundo mbinu
Posted on: Wednesday, 12 July 2023
Waziri Mkenda asisitiza kipaumbele mafunzo ya ufundi stadi sambamba na upanuzi wa miundo mbinu kwenye vyuo vya VETA.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, amesema Serikali itaendelea kutoa kipaumbele kwenye mafunzo ya ufundi stadi na kuongeza fursa zaidi za watanzania kujipatia mafunzo hayo.
Prof Mkenda ameyasema haya jana tarehe 11 Julai, 2023 alipotembelea chuo cha VETA cha Mkoa wa Tanga ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku mbili jijiji hapo.
Akiwa chuoni hapo Mhe. Mkenda amesema kwa sasa Serikali inajenga vyuo vya VETA kote nchini kuwezesha wananchi wote wanaohitaji mafunzo hayo kuyapata bila kikwazo chochote.
“Napata mrejesho kutoka kwa wananchi na ukweli ni kwamba wamefurahi sana na wananipa shukrani nipeleke kwa Mheshimiwa Rais kwa uamuzi wa kujenga VETA katika kila wilaya,”amesema
Prof Mkenda ameiagiza VETA kujipanga vizuri kukidhi matumaini ya wananchi hasa kwa kuzingatia ubora wa mafunzo yanayotolewa ili kuwezesha vijana kujipatia ujuzi unaokidhi mahitaji ya soko la ajira.
Prof. Mkenda ameahidi kuendeleza ziara zake kwenye vyuo vya VETA ili kujionea na kujiridhisha juu ya mafunzo yanayotolewa na kuahidi kuzifanyia kazi changamoto zinazokabili utoaji mafunzo.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore, amesema katika mwaka wa fedha 2022/2023 Wizara imeitengea VETA kiasi cha shilingi billion 54 ambapo tayari wameshapatiwa zaidi ya shilingi bilioni 49 kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Mamlaka hiyo.
CPA Kasore amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha VETA inapata fedha za miradi mbalimbali hasa ya mafunzo ya ufundi stadi ili kusogeza mafunzo hayo karibu na wananchi.
Pia aliishukuru serikali kwa kutoa vibali vya ajira kwa watumishi wapatao 514 ambao wameongeza tija katika mafunzo.
Katika ziara hiyo, Waziri Mkenda alitembelea karakana katika chuo hicho na kupanda mti wa kumbukumbu