The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
VETA imeweka utaratibu maalum kwa ajili ya kujiunga ili kupata mafunzo katika vyuo inavyovimiliki. Utaratibu ni kama unavyoelezwa hapa chini:
VETA hutoa mafunzo ya muda mrefu na mfupi na katika mifumo mbalimbali;
Kwa mafunzo ya muda mrefu, yyuo vyote hutangaza nafasi za kujiunga mwezi wa Agosti kila mwaka. Matangazo hutolewa katika vyombo vya habari nchini pamoja na kwenye tovuti ya www.veta.go.tz;
Mwombaji ni lazima awe amemaliza elimu ya msingi, sekondari na kuendelea;
Mwombaji huchukua fomu katika chuo chochote kilichopo karibu. Fomu hizo zina taarifa ya vyuo vyote vinavyomilikiwa na VETA, ikiwa ni pamoja na fani zinazofundishwa na mahali chuo kilipo na kama ni kutwa au bweni;
Mwombaji anaruhusiwa kufanya mtihani wa kujiunga mkoa aliochukua fomu lakini anaweza kuchagua kusoma mkoa wowote anaochagua kulingana na mahitaji yake;
Mwombaji anatakiwa kufanya mtihani wa kujiunga (Aptitude Tests) mwezi Oktoba na wale wanaofanikiwa kuchaguliwa hupewa taarifa mwezi Decemba ili kuanza masomo Januari mwaka unaofuata;
Mwombaji anayefanikiwa hupewa barua ya kujiunga inayofafanua mahitaji yote muhimu. Mahitaji yanatofautiana toka chuo kimoja hadi kingine na kutegemeana na fani aliyoomba, na pia kama ni kutwa au bweni;
Kwa utaratibu huu Mwombaji anaanza kujiunga na daraja la 1(Level 1) ambalo ni daraja la chini. Waombaji wanaoendelea madaraja ya juu (Level II-III) vigezo ni ufaulu wa daraja husika unamwezesha kupanda daraja lingine.