The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imeipatia Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) msaada wa kompyuta 50 kwa ajili ya kutolea mafunzo katika vyuo vya VETA nchini. Akizungumza baada ya kupokea kompyuta hizo, jana tarehe 19 Agosti, 2024, kwenye ofisi za VETA Makao Makuu, jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Eniart Mahundi, aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa VETA, amesema kompyuta hizo 50 zitaenda kutumika katika kutolea mafunzo ya ICT katika vyuo vya VETA.
“Kwa niaba ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) nitoe shukrani za pekee kwa BOT kwa msaada huu wa kompyuta 50 ambazo kwa sisi zitatufaa sana kwa ajili ya utoaji mafunzo kwa vijana wetu”, Amesema.