The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
CEFA YAIPA VETA DSM KOMPYUTA TISA ZA KUFUNDISHIA WATU WA MAHITAJI MAALUM
Posted on: Sunday, 02 June 2024
Shirika la Kimataifa la CEFA nchini Tanzania limekipatia chuo cha VETA Mkoa wa Dar es Salaam kompyuta tisa (9) kwa ajili ya kufundishia watu wenye mahitaji maalum.
Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar es Salaam, Wilhard Soko amepokea kompyuta hizo na kushukuru Shirika hilo kwa kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Chuo hicho kuwapatia ujuzi watu wenye mahitaji maalum.