The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Ndugu Godfrey Mnzava, ameipongeza mamlaka ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi (VETA) kwa kuendelea kuwa kinara katika utoaji wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi nchini.
Ndugu Mnzava ameyasema hayo jana tarehe 17/09/2024 alipotembelea katika banda la VETA Buhigwe kwenye mkesha wa mbio za Mwenge katika viwanja vya shule ya msingi Buhigwe katika Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma.
Ndugu Mnzava amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi kote nchini.
“Natoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa za kujiunga na mafunzo ya ufundi stadi ili kupata ujuzi kwa maendeleo binafsi na Taifa," Mnzava amesisitiza.
Aidha ameiagiza mamlaka ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi (VETA) kupitia Chuo cha VETA Buhigwe, kuongeza hamasa katika kutangaza chuo hicho ili kuongeza idadi ya udahili wa wanafunzi.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Buhigwe, Ndugu Ally Bushiri amesema, Chuo cha VETA Buhigwe ni kipya ambacho kina uwezo wa kuchukua wanafunzi 240, lakini hadi sasa chuo kina wanafunzi 86 tu.