The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
MASHINDANO YA UMAHIRI YAWA KIVUTIO WIKI YA UBUNIFU
Posted on: Wednesday, 26 April 2023
MASHINDANO YA UMAHIRI YAWA KIVUTIO WIKI YA UBUNIFU
Mashindano ya Umahiri katika Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa wanafunzi wa VETA yaliyofanyika tarehe 25 Aprili 2023 katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, yamevutia wananchi wengi wanaliotembelea Wiki ya Ubunifu katika Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma.
Mashindano hayo VETA yalifanyika Siku Maalum ya VETA (VETA Day) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Ubunifu Kitaifa inayofanyika tarehe 25 hadi 28 Aprili 2023.
Mashindano hayo yameshirikisha wanafunzi kutoka katika fani nne za ufundi stadi ambazo ni Uashi, Umeme, Elektroniki pamoja na Ususi na Urembo.
Washindu watatu kwenye kila fani walitunukiwa vyeti vya Ushindi pamoja na fedha taslimu na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika hafla ya utoaji zawadi kwa washindi hao.
Katika fani ya Ususi na Urembo, mshindi wa kwanza alikuwa Ester Lihweuli kutoka chuo cha VETA Shinyanga, akifuatiwa na Happiness Mponda kutoka chuo cha VETA Dodoma (nafasi ya pili) na Gladness Malaki kutoka chuo cha High Score Dododma aliyeshika nafasi ya tatu.
Katika fani ya Ufundi Uashi mwanafunzi Anord Brighton kutoka chuo cha VETA Kagera aliibuka mshindi wa kwanza akifuatiwa na Mustapha Bakari kutoka chuo cha VETA Lindi (nafasi ya pili) na Kelvin Teete wa chuo cha Ufundi Stadi Don Bosco Dodoma, nafasi ya tatu.
Mwanafunzi Joseph Nusuhela kutoka chuo cha VETA Songea alikuwa mshindi wa kwanza katika fani ya Ufundi Umeme akifuatiwa na Happy Nyamwela kutoka VETA Dodoma (nafasi ya pili), na Baraka Mwaisaka kutoka chuo cha VETA Kihonda alishika nafasi ya tatu.
Fani ya Elektroniki, Eliud Modest, mwanafunzi kutoka chuo cha VETA Kipawa alishika nafasi ya kwanza mbele ya Robert Robert kutoka chuo cha VETA Dar es salaam (wa pili) na Selemani Juma kutoka chuo cha VETA Pwani, nafasi ya tatu.
Watu wengi walioshuhudia mashindano hayo wasema kuwa ni jambo la kuvutia na la kipekee katika kuonesha namna wanafunzi walivyoiva katika fani zao.
Walishauri utaratibu huo wa mashindano ya ubunifu uendelezwe katika maonesho mengine na kupanua wigo wa fani na washiriki.