The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
MBUNGE AAHIDI MKOPO WA PIKIPIKI 200, BAJAJI 10 KWA WAHITIMU WA UDEREVA VETA MARA
Posted on: Sunday, 10 March 2024
MBUNGE AAHIDI MKOPO WA PIKIPIKI 200, BAJAJI 10 KWA WAHITIMU WA UDEREVA VETA MARA
Mbunge wa Musoma Mjini, Mhe. Vadastus Mathayo, ameahidi kuwawezesha mkopo wa pikipiki 200 na bajaji 10 wahitimu wa udereva wa chuo cha VETA Mara.
Mhe. Mathayo ametoa ahadi hiyo wakati wa mahafali ya wahitimu 220 wa udereva wa bodaboda na bajaji yaliyofanyika tarehe 9 Machi,2024 katika chuo Cha VETA Mara ambapo Mbunge huyo alikuwa Mgeni Rasmi.
Mahafali hayo yalihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Musoma Mhe.Dkt. Khalfan Haule, Mstahiki Meya wa Musoma Mjini Mhe. William Gumbo na viongozi wengine Wilayani hapo ambao wamempongeza Mbunge huyo kwa kufadhili mafunzo kwa madereva hao.
Mkuu wa Wilaya Mhe. Dkt. Khalfan Haule amewahimiza madereva hao kuzingatia yote waliyojifunza na kuagiza chuo hicho kuanzisha kozi ya ukarimu kwa ajili ya kuhudumia mbuga ya Taifa Serengeti.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Mara, Martin Mollel amesema chuo chake kitaimarisha utoaji mafunzo kwenye sekta ya utalii na ukarimu.
Amesema chuo hicho kimeanzisha kozi za muda mfupi za Uandaaji Chakula, Mauzo na Huduma ya Chakula na Vinywaji, Uhazili pamoja na TEHAMA ambapo amewakaribisha wananchi kujipatia mafunzo katika Chuo cha VETA Mara.