The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
MHE. SEKIBOKO AFURAHISHWA NA UMAHIRI WA WANAFUNZI WA VETA
Posted on: Saturday, 20 May 2023
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, Mhe. Husna Sekiboko (Mb) ametembelea banda la VETA kwenye Maonesho ya Pili ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi na kuvutiwa na umahiri wa wanafunzi wa VETA katika kueleza na kufafanua vyema kile walichojifunza kwenye fani zao.
Akiwa kwenye Banda hilo, Mhe. Sekiboko amepongeza ubunifu wa miwani ya kuzuia madereva kusinzia barabarani uliofanywa na mwalimu na mwanafunzi wa chuo cha VETA Dodoma na kuitaka VETA kusimamia uendelezaji wa ubunifu huo ili uingie rasmi kwenye matumizi.
“Fanyeni jitihada ubunifu huu uingie kwenye matumizi… yaani hii naisubiria kwa hamu sana na nitakuwa mteja wa kwanza,”amesema