The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
Mkurugenzi Mkuu TLSB aiomba VETA kuandaa machapisho na kuyaweka maktaba
Posted on: Saturday, 06 July 2024
Mkurugenzi Mkuu TLSB aiomba VETA kuandaa machapisho na kuyaweka maktaba
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania, Dkt. Mboni Ruzegea, ameiomba Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), kuandika machapisho ya taarifa za shughuli zake ikiwemo za ubunifu na kuziweka katika maktaba nchini.
Dkt. Ruzegea ametoa wito huo leo Julai 3, 2024, alipotembelea banda la VETA katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Dar es salaam (Sabasaba).
"Kwa kufanya hivyo mtakuwa mnatangaza huduma zenu, kwani watu wengi hutumia muda wao wa likizo kwenda maktaba kujisomea," amesema.
Amesema ameona tofauti kubwa katika banda la VETA ukilinganisha na maonesho ya Sabasaba yaliyopita.
“Nyinyi kama taasisi mmeweza kupanua huduma zenu hasa kwenye huu upande wa watu wenye mahitaji maalum,” amesema.
Monesho ya Sabasaba
yamefunguliwa rasmi leo, tarehe 3 Julai 2024 na Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Filipe Nyusi akiambatana na mwenyeji wake Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na yatafikia kilele tare 13 Julai 2024.