Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dkt. Pancras Bujulu, amekutana na wanahabari wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa Dar es Salaam (DCPC) na kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali juu ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, yakiwemo utoaji wa mafunzo na fursa za mafunzo hayo kwa Watanzania, mchango wa VETA kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii, ubunifu na uanzishaji wa viwanda vidogo na vya kati, na nafasi ya wanahabari kwa maendeleo na ustawi wa VETA.
Katika mkutano huo, uliofanyika katika ofisi za VETA Makao Makuu jijini Dar es Salaam leo tarehe 17 Oktoba 2020, Dkt. Bujulu amewasihi waandishi hao kuendelea kuandika, kutangaza na kueneza habari zinazohusu Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini ili kusaidia umma kupata uelewa wa kutosha na kunufaika na fursa zilizopo VETA.
Dkt. Bujulu ametumia fursa hiyo kuwakaribisha waandishi hao kupata mafunzo ya stadi mbalimbali na kutembelea vyuo vya VETA ili kujionea kinachofanyika, kufanya mahojiano na kupata taarifa rasmi za Mamlaka na kisha kutangaza au kuandika habari na makala ili umma uzidi kuelimika zaidi.
VETA HEAD OFFICE,
12 VETA Road.
41104 Tambukareli,
P.O. BOX 802, Dodoma Tanzania,
Email: info@veta.go.tz
Telephone: +255 26 2963661
Fax: +255 22 2863408
Url: www.veta.go.tz
© 2018 - VETA Head Office