Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam Malima jana tarehe 7 Agosti, 2020 ametembelea banda la VETA kwenye maonesho ya Nanenane kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi wilayani Bariadi, Simiyu na kufurahishwa na ubunifu wa walimu na wanafunzi wake.
Akiwa katika banda la VETA ambapo alijionea ubunifu wa teknolojia mbalimbali alisema amevutiwa na namna ambavyo VETA imebeba vyema majukumu yake.
"Kimsingi hili ndilo jukumu la VETA na mnapaswa kuliendeleza. VETA inatakiwa mara kwa mara kuangalia changamoto za jamii na kubuni teknolojia na vitu mbalimbali kutoa suluhisho la changamoto hizo".Alisema
Miongoni mwa ubunifu aliovutiwa nao ni mashine ya kutotolesha vifaranga inayotumia mafuta ya taa, kitanda tiba, benchi lenye matumizi mbalimbali (Benchi meza mkunjo) na mashine ya kuzidua unga wa ubuyu.
Mhe. Malima aliagiza kutengenezewa benchi meza mkunjo mbili.
VETA HEAD OFFICE,
12 VETA Road.
41104 Tambukareli,
P.O. BOX 802, Dodoma Tanzania,
Email: info@veta.go.tz
Telephone: +255 26 2963661
Fax: +255 22 2863408
Url: www.veta.go.tz
© 2018 - VETA Head Office