Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina ametembelea banda la VETA kwenye maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Nyakabindi Wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Akiwa kwenye banda la VETA, Waziri Mpina amefurahishwa na shughuli zinazofanywa na VETA katika kuboresha sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Waziri huyo ameiagiza VETA kupitia Chuo cha VETA Singida kuandaa mafunzo ya ufugaji bora wa kuku kwa Kikundi cha Wakulima cha Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu na kuwapatia wananchi Majogoo 100 wa Kienyeji kwa ajili ya kuanza ufugaji.
Waziri huyo pia alivutiwa na Mashine ya Kuzidua Ubuyu iliyobuniwa na Mwalimu wa Chuo cha VETA Kihonda na kuagiza mashine hiyo itengenezwe na kupatiwa kwa Wakulima wa Ubuyu wa Wilaya hiyo ili kurahisisha utengenezaji wa bidhaa zinazotokana na unga wa Ubuyu.
VETA HEAD OFFICE,
12 VETA Road.
41104 Tambukareli,
P.O. BOX 802, Dodoma Tanzania,
Email: info@veta.go.tz
Telephone: +255 26 2963661
Fax: +255 22 2863408
Url: www.veta.go.tz
© 2018 - VETA Head Office