The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
MWENGE WA UHURU KITAIFA WAZINDUZIA KLABU YA WAPINGA RUSHWA VETA NAMTUMBO
Posted on: Friday, 21 April 2023
Mwenge wa Uhuru Kitaifa ukiongozwa na Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa, Ndugu Abdalla Shaib Kaim, ulizindua Klabu ya Wapinga Rushwa katika Chuo cha VETA Namtumbo, siku ya Jumanne, tarehe 18 Aprili 2023. Lengo la klabu hiyo ni kuwajengea maadili mema na kuwaandaa vijana kuwa wazalendo kwa nchi yao na kwa taifa kwa Ujumla.
Viongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru wakiwa chuoni hapo pia walipata fursa ya kupanda miti ya kumbukumbu ya wakimbiza Mwenge kitaifa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa klabu hiyo kiongozi wa mbio za Mwenge aliwapongeza walimu na wanafunzi wa chuo cha VETA kwa kuanzisha klabu hiyo na kuwataka kuendelea kupeana elimu juu ya athari za rushwa na namna ya kuzuia na kupambana na rushwa.
“Natambua rushwa ni adui wa haki na ni adui wa maendeleo. Muendelee kuwa wazalendo na wadau wazuri wa kupambana na rushwa.”