The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
MWENGE WA UHURU WAZINDUA KLABU ZA KUPAMBANA NA RUSHWA, KUPINGA DAWA ZA KULEVYA VETA DODOMA
Posted on: Tuesday, 03 October 2023
MWENGE WA UHURU WAZINDUA KLABU ZA KUPAMBANA NA RUSHWA, KUPINGA DAWA ZA KULEVYA VETA DODOMA
Mwenge wa Uhuru Kitaifa umezindua klabu ya kuzuia na kupambana rushwa na klabu ya kupinga matumizi ya dawa za kulevya katika chuo cha VETA Dodoma.
Akisoma taarifa kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa, Ndugu Abdalla Shaib Kaim leo tarehe 3 Oktoba, 2023, Kiongozi wa klabu ya kupambana na rushwa chuoni hapo Ndg. Andason Hongoli, amesema lengo la klabu hizo ni kutoa elimu kwa vijana juu ya madhara ya rushwa na dawa za kulevya.
Amesema klabu hizo pia zitashiriki kikamilifu katika kuhamasisha vijana kushiriki na kusimama imara kwenye mapambano dhidi ya rushwa na matumizi ya dawa za kulevya na kutoa taarifa za vitendo hivyo.
“Klabu hizi zitawezesha kutoa taarifa za vitendo vya rushwa, dawa za kulevya na kuwa tayari kutoa ushahidi mahakamani dhidi ya watakaobainika na makosa kama hayo hapa chuoni na nje ya chuo,”amesema
Ndg. Hongoli amesema klabu hizo zilizoanzishwa chini ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma kwa kushirikiana na Uongozi wa Chuo cha VETA Dodoma, zina jumla ya wanachama 73 ambapo 50 ni wa klabu ya kuzuia na kupambana na rushwa na 23 ni wa klabu ya kupinga dawa za kulevya.