The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
MWENYEKITI WA BARAZA NACTVET AIPONGEZA VETA UWEZESHAJI UJUZI KWA MAKUNDI MAALUM
Posted on: Friday, 05 July 2024
MWENYEKITI WA BARAZA NACTVET AIPONGEZA VETA UWEZESHAJI UJUZI KWA MAKUNDI MAALUM
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), Bi. Bernadetta Ndunguru, ameipongeza VETA kwa kutoa ujuzi kwa makundi maalum hasa watu wenye ulemavu na kuwawezesha kujiajiri na kujipatia kipato.
Bi. Ndunguru ametoa pongezi hizo leo tarehe 5 Julai, 2024, alipotembelea banda la VETA kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam na kupata taarifa za utoaji mafunzo pamoja kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na wanafunzi, walimu na wahitimu wa VETA.
“Kwa kweli VETA mnafanya kazi kubwa sana na mnaonesha ni jinsi gani kila Mtanzania na hasa watu wenye mahitaji maalumu wanaweza kupata mafunzo ya ufundi stadi wakawa na ujuzi unaowawawezesha kujitegemea,” amesema
Bi. Ndunguru pia amepongeza uanzishwaji wa mtaala wa kufundisha wafanyakazi wa majumbani kwa kuwa wafanyakazi hao watapata ujuzi na kuwawezesha kutambulika na hatimaye kufanya kazi zao kwa kujiamini na kwa ufanisi zaidi.
Amewahimiza wazazi wenye watoto wenye mahitaji maalum kujitokeza na kuwapeleka watoto wao kwenye vyuo vya ufundi stadi kujipatia ujuzi na kuondoa dhana kuwa watoto hao hawafundishiki.