The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
Naibu Waziri TAMISEMI azungumzia umuhimu wa upanuzi wa fursa za mafunzo ya ufundi stadi
Posted on: Saturday, 06 July 2024
Naibu Waziri TAMISEMI azungumzia umuhimu wa upanuzi wa fursa za mafunzo ya ufundi stadi
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI anayeshughulikia Elimu, Mhe. Zainabu Katimba, amesema upanuzi wa fursa za mafunzo ya ufundi stadi kwa watanzania utawezesha kuzalisha mafundi mahiri na wa kutosha wanaohitaji kwa wingi kuendesha shughuli za uzalishaji na kukuza uchumi.
Mhe. Katimba amesema hayo tarehe 5 Julai, 2024, alipotembelea banda la VETA kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam na kujionea shughuli mbalimbali za utoaji mafunzo ya ufundi stadi zinazofanywa na VETA.
Amesema ipo haja ya kufanya uwekezaji katika vyuo vya ufundi stadi ili kutoa fursa ya wananchi kujipatia ujuzi hasa kwa kuzingatia uhitaji mkubwa wa mafundi hayo kwenye soko la ajira na kupongeza juhudi za Serikali katika kuhakikisha kila Wilaya inakuwa na Chuo cha VETA.
Mhe. Katimba pia ameeleza kufurahishwa kwake na uwezo wa watu weye mahitaji maalum katika kufanya shughuli za kiufundi na kupongeza VETA kwa kazi kubwa wanayofanya ya kutoa ujuzi kwa makundi yote kwenye jamii.
“Nimetembelea banda la VETA hapa Sabasaba na kujionea bunifu mbalimbali, pia nimejionea mtu mwenye ulemavu wa macho akitengeneza bidhaa nzuri kwa kutumia mbao… nimejionea pia watu wenye ulemavu wa wakiwa na ujuzi wakitengeneza mkaa na wanaweza kujitegemea kwa kujiajiri wenyewe,” amesema.