The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
Ndalichako (Mb) ametembelea banda la VETA kwenye Maonesho NACTVET 2023
Posted on: Friday, 19 May 2023
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Prof. Joyce Ndalichako (Mb) ametembelea banda la VETA kwenye Maonesho ya Pili ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi yanayofanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
VETA inashiriki maonesho hayo ikiwa ni sehemu ya kutoa taarifa kwa jamii juu ya fursa za elimu na mafunzo ya ufundi stadi zinazopatikana kwenye vyuo vyake nchini na kuhamasisha wananchi hasa vijana kujiunga na mafunzo hayo ili kujipatia ujuzi utakaowawezesha kuajirika.
Maonesho hayo yaliyoanza tarehe 16 Mei, 2023 yanatarajiwa kumaliza tarehe 22 Mei 2023 na yanaongozwa na kauli mbiu “Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa Nguvukazi Mahiri”