Tarehe 7 Agosti, 2020 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), William Erio, akiambatana na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Prof. Raphael Chibunda wametembelea banda la VETA kwenye maonesho ya Nanenane kitaifa wilayani Bariadi,Simiyu na kupongeza juhudi zinazofanywa na VETA katika kuandaa nguvu kazi yenye ujuzi.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF alihimiza VETA kuendelea kuhamasisha wajasiriamali kuendelea kutumia fursa za mikopo ya NSSF inayotolewa kwa ushirikano na VETA, SIDO, NEEC na Benki ya Azania .
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha SUA alihimiza VETA kutoa mafunzo kwa vitendo yanayoambatana na uzalishaji
VETA HEAD OFFICE,
12 VETA Road.
41104 Tambukareli,
P.O. BOX 802, Dodoma Tanzania,
Email: info@veta.go.tz
Telephone: +255 26 2963661
Fax: +255 22 2863408
Url: www.veta.go.tz
© 2018 - VETA Head Office