The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe.Prof. Adolf Mkenda, akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA. Anthony Kasore juu ya utoaji wa mafunzo ya ufundi stadi pamoja na ubunifu alipotembelea banda la VETA kwenye Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu tarehe 27 Mei, 2024.
Mhe. Mkenda amepongeza utoaji wa mafunzo kuendana na mahitaji ya soko la ajira na kuonesha kuvutiwa na mafunzo ya Mekatroniki yanayotolewa katika Chuo cha VETA Kipawa pamoja na mafunzo kwa wafanyakazi wa majumbani yaliyoanza kutolewa katika vyuo vya VETA Tanga na Dodoma.
Akiwa kwenye banda la VETA, Mhe. Mkenda amempongeza Mwalimu wa Chuo cha VETA Kigoma Innocent Maziku kwa kubuni kifaa cha kusaidia kuongeza usikivu kwa watu wenye usikivu hafifu na kutoa wito kwa Taasisi na wadau wanaohusika na uendelezaji ubunifu nchini kuwezesha ubunifu huo kufikia wahitaji ikiwemo wanafunzi wenye changamoto hiyo.
VETA inashiriki kwenye Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu jijini Tanga ambapo Mhe. Mkenda amefungua rasmi maadhimisho hayo yaliyoanza tarehe 25 Mei 2024 na yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 31 Mei, 2024.