Tarehe 30 Juni, 2020, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako, ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Kasulu, kinachojengwa katika Halmashauri ya Mji Kasulu, mkoani Kigoma.
Katika ziara hiyo Prof. Ndalichako aliongozana na Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini Mh. Daniel Nswanzugwako, Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Simon Anange, Mwenyekiti wa Bodi ya Elimu na Ufundi Stadi Ndg. Peter Maduki, Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dkt. Pancras Bujulu, Wajumbe wawili wa Bodi ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Dkt. Ethel Kasembe na Dkt.Michael Mawondo, pamoja na viongozi wengine wa Chama na Serikali ya Wilaya ya Kasulu.
Ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Kasulu unatekelezwa na Halmashauri ya Mji Kasulu na kusimamiwa na Mshauri Elekezi, Chuo cha Ufundi Arusha, kwa gharama ya shilingi bilioni 2.19 chini ya Mradi wa Kukuza Elimu na Ujuzi kwa kazi zenye tija (ESPJ).
Ujenzi wa Chuo hicho unatarajiwa kukamilika mwezi Septemba 2020.
VETA HEAD OFFICE,
12 VETA Road.
41104 Tambukareli,
P.O. BOX 802, Dodoma Tanzania,
Email: info@veta.go.tz
Telephone: +255 26 2963661
Fax: +255 22 2863408
Url: www.veta.go.tz
© 2018 - VETA Head Office