Mkurugenzi Mkuu wa VETA anawatangazia Wananchi wote nafasi za kujiunga na Kozi za Muda Mrefu katika Vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi vinavyomilikiwa na VETA.
FOMU
Fomu za kujiunga zitatolewa kuanzia tarehe 3 Agosti hadi 18 Septemba, 2020 katika Vyuo vyote vya VETA nchini. Gharama ya fomu ni Shiling 5,000 tu.
SIFA ZA KUJIUNGA
• Umri ni kuanzia miaka 15 na kuendelea; na
• Kuanzia ngazi ya elimu ya msingi na sifa za ziada kwa baadhi ya fani zimebainishwa kwenye fomu ya maombi.
ADA NA GHARAMA ZA MAFUNZO
Ada za mafunzo kwa kozi za muda mrefu kwa vyuo vinavyomilikiwa na VETA kwa sasa ni shilling 60,000/= (elfu sitini) kwa mwanafunzi wa kutwa kwa fani zote na shilling 120,000/=(laki moja na elfu ishirini) kwa mwanafunzi wa bweni kwa mwaka. Gharama zingine hutegemeana na mahitaji mahsusi ya fani husika.
Pamoja na tangazo hili tumeambatisha orodha ya Vyuo na fani zitakazotolewa.Fungua hapa kupata orodha
Aidha, utaratibu wa maombi ya kujiunga na Vyuo vingine vilivyosajiliwa na VETA utapatikana katika Ofisi za Kanda kama ilivyo kwenye kiambatisho. Fungua hapa
Tangazo hili limetolewa na
Sitta Peter
Meneja Uhusiano.
Tarehe 23 julai, 2020
VETA HEAD OFFICE,
12 VETA Road.
41104 Tambukareli,
P.O. BOX 802, Dodoma Tanzania,
Email: info@veta.go.tz
Telephone: +255 26 2963661
Fax: +255 22 2863408
Url: www.veta.go.tz
© 2018 - VETA Head Office