Katika kuadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma tarehe 16 hadi 23 Juni mwaka huu, Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA, itafungua milango katika ofisi zake za Makao Makuu, kwenye vyuo na kanda ndani ya wiki hiyo kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya mafunzo na huduma zinazotolewa pamoja na kujibu na kufafanua hoja mbalimbali kutoka kwa wananchi.
Tunawakaribisha wananchi kwa wingi kutembelea ofisi na vyuo vyetu ndani ya wiki hiyo kuanzia saa 7.00 mchana hadi saa 11.30 jioni ambapo pamoja na kupata elimu kuhusu mafunzo na huduma zetu, pia wapewa fursa ya kutembelea karakana za vyuo na kujionea namna mafunzo yanavyoendeshwa.
Vilevile, tunakaribisha maoni na hoja mbalimbali kutoka kwa wadau na wananchi kwa watakaoshindwa kufika katika ofisi za VETA kupitia anuani zifuatazo VETA Makao Makuu, S.L.P. 2849, Dar es Salaam, Baruapepe: info@veta.go.tz au pr@veta.go.tz Simu: +255 22 2863409 Wote mnakaribishwa
VETA HEAD OFFICE,
12 VETA Road.
41104 Tambukareli,
P.O. BOX 802, Dodoma Tanzania,
Email: info@veta.go.tz
Telephone: +255 26 2963661
Fax: +255 22 2863408
Url: www.veta.go.tz
© 2018 - VETA Head Office