The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
TIMU YA VETA MAKAO MAKUU YAENDELEZA UBABE: YAILAZA TUME YA UTUMISHI WA UMMA 1-0
Posted on: Saturday, 14 September 2024
Timu ya mpira wa miguu VETA Makao Makuu imeendelea kuonesha ubabe katika michezo ya kirafiki inayofanyika ikiwa ni mwendelezo wa maandalizi ya ushiriki kwenye mashindano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma,Taasisi na Makampuni Binafsi ( SHIMUTA).
Jana, Ijumaa, tarehe 13 Septemba 2024, VETA Makao Makuu imejinyakulia ushindi wa goli 1-0 dhidi ya timu ya Tume ya Utumishi wa Umma katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye viwanja vya Killimani Uzunguni, jijini Dodoma.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa wa aina yake, timu zilienda mapumziko zikiwa hazijapata kitu, licha ya nafasi nyingi kutengenezwa.
Kipindi cha pili kilianza huku timu zote zikionesha kuhitaji ushindi kwenye mchezo huo, VETA ikapata bao kupitia kwa Juma Nassari na kuwainua mashabiki wa VETA.