The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
UWEKAJI JIWE LA MSINGI LA MRADI WA UJENZI WA CHUO CHA UFUNDI STADI CHA WILAYA YA RUANGWA
Posted on: Thursday, 12 August 2021
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), tarehe 7 Juni 2021 ameweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.
Mradi huo unatekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kwa kusimamiwa na Mshauri Elekezi, Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), kwa gharama ya shilingi bilioni 2.2 kwa fedha za Mradi wa Kukuza Elimu na Ujuzi kwa Kazi zenye Tija (ESPJ).
Chuo hicho kitakapokamilika kitakuwa na uwezo wa kudahili wanafunzi 560 kwa mwaka katika fani za ufundi umeme, Useremala, Uungaji na Uchomeleaji vyuma, Uashi, Ushonaji na Mitindo ya Mavazi, Usindikaji Vyakula na TEHAMA.
Kazi Inaendelea kukamilisha ujenzi wa vyuo vingine 30 vya ufundi stadi nchini.