The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
VETA Iringa ladies imeaga mashindano ya ligi ya mabingwa wa mikoa wanawake baada ya kukubali kufungwa mabao tatu kwa moja na timu ya Simba Queens ya mkoani Kilimanjaro, hapo jana tarehe 24 Juni 2024 katika viwanja vya Fontain Gate Academy, Jijini Dodoma.
VETA Iringa Ladies imeshia katika hatua ya makundi ikishika nafasi ya tatu katika kundi lililokuwa na timu tano huku ikishinda mechi mbili na kupoteza mechi mbili.
Akizumnguza kwa niaba ya timu, leo tarehe 25 Juni 204, mara baada ya kupita Makao Makuu ya VETA kwa ajili yakuaga na kutoa shukurani zao kutokana na ushirikiano walioupata kutoka kitengo cha Uhusiano kwa Umma, kocha wa timu hiyo, mwalimu Laison Tuyebe amesema japo wametolewa katika kinyang'anyiro hicho hawatakata tamaa kushiriki katika mashindano mengine.
“tumepita hapa leo kutoa shukurani zetu za dhati kwa ushirikiano mliotupa tangu tumeanza mashindano haya na sasa tujanarejea mkoani Iringa,” amesema kocha Laison
Kwa upande wake Mkurugenzi wa timu ya VETA Iringa Ladies, Ramadhani Mahano amesema kutokusonga kwao mbele kumechagizwa na kukosekana kwa wachezaji ambao wanaunda timu hiyo, wengi wakiwa ni wanafunzi wa mwaka wa tatu na mwaka wa pili ambao katika kipindi hiki cha ligi wao wapo maeneo mbalimbali wakifanya mafunzo kwa vitendo hivyo wameshindwa kushiriki.
“Tumelazimika kuchukua wanafunzi wa mwaka wa kwanza kushiriki katika ligi hii kwani wanafunzi wa mwaka wa pili na mwaka wa tatu ambao ndio waozefu wapo maeneo mbalimbali wakijfunza kwa vitendo,” amesema Ramadhani Mahano.
Timu ya VETA Iringa Ladies imerejea salama leo mkoani Iringa.