The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
VETA Iringa ladies yaicharaza timu ya Nguruka bao nne
Posted on: Tuesday, 25 June 2024
VETA Iringa ladies yaicharaza timu ya Nguruka bao nne
VETA Iringa ladies, leo tarehe 21 Juni 2024, imeonyesha ubabe wake mbele ya timu ya Nguruka kutoka Kigoma kwa kuitandika mabao 4 kwa moja, katika viwanja vya fontain gate, Jijini Dodoma.
Akizumnguza kwa bashasha baada ya kumalizika kwa mchezo huo, kocha wa timu ya VETA Iringa lades, mwalimu Laison Tuyebe amesema matokeo ya jana yaliwafanya kukosa usingizi na kujifua zaidi siku ya leo, hatimaye wamemaliza mechi kwa ushindi mnono.
“leo tumetoka kifua mbele na wachezaji bado wana afya njema na ari ya kuendelea kushinda katika mechi yetu tutakayocheza siku ya Jumapili,” amesema kocha Laison
Kwa upande wake Mwenyekiti wa timu ya VETA Iringa Ladies, Guntramu Kawonga amesema matokeo ya jana yalifanya aongee na wachezaji hao baada ya kufanya vibaya jana na kufungwa goli moja kwa nunge.
“kama tutafanikiwa kushinda michezo miwili iliyo salia basi tutatinga hatua ya nusu fainali katika ligi hii,” amesema.
Mwenyekiti huyo pia amekishukuru kitengo cha Uhusiano kwa Umma cha VETA kwa kuendelea kuhabarisha umma juu ya ushiriki wa VETA Iringa Ladies katika ligi hiyo kwani kwa kufanya hivyo kunaitangaza Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi.
Kwa upande wachezaji wanaendelea kujifua zaidi ilikupata ushindi kama wa leo.
Magoli ya timu ya VETA Iringa Ladies yamefungwa na Anita Sokole dk ya 30, Zainabu Mbaruku dk ya 44, Lidya Gyee dk ya 79 na hatimaye katika dk 2 za nyongeza Machina Yangi akafunga bao la nne baada ya dk 90 za mchezo kumalizika.
Mashindano hayo yameanza tarehe 20 Juni Jijini Dodoma na yatahitimishwa tarehe 29 Juni 2024.