The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
Mhitimu wa fani ya mavazi na ubunifu wa nguo kutoka chuocha VETA Songea Riziki Ndumba akichukua vipimo vya nguo kwaajili ya kumshonea nguo Esther Peter Mgale mkazi wa ubungo Jijini Dar es salaam baada ya kutembelea banda la VETA katika viwanja vya J.K. Nyerere tarehe 29 Juni 2024.
Esther Mgale amejikuta akipigwa na butwaa baada ya kuona Riziki mwenye ulemavu wa viungo ana uwezo mkubwa wa kushona nguo bila kuhitaji msaada wa mtu mwingine kuanzia hatua za upimaji wa vipimo vya nguo, kukata nguo kwa kutumia mkasi, kutunga uzi kwenye sindano na hatimaye kushona nguo iliyokamilika.
“kwa kweli nimepatwa na mshangao kumuona kijana Riziki akiweza kushona nguo bila kuhitaji msaada wa mtu mwingine , kweli hii nimara yangu ya kwanza kuja kwenye maonesho haya, nawasihii wakazi wenzangu wa Dar es salaam wafike katika banda la VETA kuna vitu vizuri” amesema Esther
VETA wapo katika maonesho hayo tangu tarehe 28 Juni mpaka yatakapo fikia kilele chake tarehe 13 Julai 2024.