The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
Tarehe 12 Mei, 2022 Wafanyakazi wa VETA Makao Makuu wameshiriki kwenye Semina ya VVU, UKIMWI na magonjwa sugu yasiyoambukiza.
Semina hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa chuo cha VETA Dodoma ilifunguliwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA. Anthony Kasore.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo, CPA Kasore amesema Serikali imeweka mpango wa watumishi kupatiwa elimu ya afya zao na kupima ili kuweza kutambua, kulinda na kuhudumia afya zao, hivyo kuwasaidia kutekeleza vyema majukumu yao kazini.
Amewasihi watumishi hao kuzingatia na kufuata maelekezo na ushauri watakaopewa na wataalam hao ili kuweza kutunza vyema afya zao.
Kasore ametumia fursa hiyo kuwakumbusha watumishi umuhimu wa kufanya mazoezi katika kuimarisha afya zao.
Naye Mtaalam wa afya kutoka Kituo cha Afya cha Makole, Dkt. Salma Gwasa ameipongeza Menejimenti ya VETA kwa kuwapatia nafasi ya kutoa elimu hiyo na kuendesha zoezi la upimaji wa afya kwa wafanyakazi.
Dkt. Salma amewasisitiza wafanyakazi kupima afya mara kwa mara kwa kuwa itasaidia kujikinga na magonjwa na kupata tiba pale wanabobainika kuwa na tatizo la kiafya.