The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
VETA, TET zakutanisha wataalamu kuandaa miongozo na vitini
Posted on: Wednesday, 08 November 2023
VETA, TET zakutanisha wataalamu kuandaa miongozo na vitini kwa ajili ya utekelezaji wa mitaala ya Sekondari Mkondo wa Amali.
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) zimekutanisha wataalamu 147 kuandaa Vitini na Miongozo kwa ajili ya utekelezaji wa mtaala wa Sekondari hatua ya chini Mkondo wa Amali, kidato cha kwanza mpaka cha nne.
Kikao kazi hicho kinachofanyika mkoani Morogoro kilianza tarehe 30 October 2023 na kinatarajiwa kuhitimishwa tarehe 30 Novemba 2023.
Kikao kazi kimehusisha washiriki 147 kutoka sehemu mbalimbali ikiwemo Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, NACTVET, TAMISEMI, Vyuo vya Ufundi Stadi, Shule za Sekondari za Ufundi, Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi, Vyuo Vikuu na vya kati na Taasisi Binafsi.
Hadi sasa ambapo Miongozo mitatu ( Mwongo wa Utoaji Mafunzo ya Amali, Mwongozo wa Utaini na Utunuku, na Mwongozo wa Kazi Mradi) na Vitini 39 vya masomo vimeandaliwa.
Akizungumza leo tarehe 7 Novemba, 2023 alipotembelea kikosi kazi cha watu wanaofanyakazi ya kuandaa Miongozo na Vitini hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dkt. Prosper Mgaya alisema ni mategemeo yake kuwa kazi hiyo itafanyika kwa ufanisi na kukamilika kwa wakati ili kuwezesha utekelezaji wa mtaala huo mpya mwaka 2024 katika mkondo wa amali.
Mgaya amesema katika kutekeleza mitaala hiyo upande wa Amali, VETA imepewa jukumu la kuratibu ufundishaji wa masomo yanayohusiana na ujuzi na kuhakikisha utekelezaji wake unakwenda kama ilivyokusudiwa.
Mafunzo ya Amali yanalenga kumpa mwanafunzi ujuzi na umahiri cha ufundi stadi, ili hatimaye aweze kutunukiwa vyeti vya Kitaifa vya Ufundi Stadi, ambapo NVA ngapi ya pili atapata akiwa kidato cha tatu na NVA ngapi ya tatu atapata akiwa kidato cha Nne.
“Tunaamini mwanafunzi huyu wa kidato cha nne baada ya kupata mafunzo haya ya Amali baada ya kumaliza shule watakuwa na uwezo wa kwenda kufanya kazi ya kuajiriwa au kujiajiri,” amesema.
Dkt Mgaya ameishukuru Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kuwezesha kufanikisha zoezi hilo hapa na kusisitiza kuwa VETA iko tayari kuhakikisha kwamba utekelezaji wa mtaala mpya unaenda sawasawa na malengo ya Serikali.