The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, ameikabidhi Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi(VETA) vishikwambi 996 kwa lengo la kurahisisha mafunzo vyuoni hasa katika eneo la Tehama.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo tarehe 4 Novemba, 2022 katika ukumbi wa Jiji la Dodoma uliopo Mtumba jijini Dodoma kwenye hafla ya uzinduzi wa ugawaji vishikwambi kwa walimu nchini.
Mhe. Majaliwa amezindua mpango huo ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Sera ya Taifa inayoakisi Mpango wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan wa Maendeleo ya Taifa ya Awamu ya Tatu ulioanza mwaka 2020/2021 na unatarajiwa kukamilika mwaka 2025/2026.
Mpango huu utawawezesha vijana walio vyuoni kupata na kuzalisha ajira na kuongeza kasi ya teknolojia ambayo nchi inaiwekea mkazo kwa sasa.
Hafla hiyo ya uzinduzi imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali akiwemo Waziri wa Elimu na Sayansi na Teknolojia, Mhe. Profesa Adolf Mkenda, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA Anthony Kasore na Mkuu wa Chuo cha Ufundi Sradi na Huduma cha Mkoa wa Dodoma Ndugu Stanslaus Ntibara.