The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
VETA yapongezwa kwa mwitikio mkubwa zoezi la upandaji miti siku ya kuzaliwa kwa Rais Samia
Posted on: Sunday, 09 February 2025
VETA yapongezwa kwa mwitikio mkubwa zoezi la upandaji miti siku ya kuzaliwa kwa Rais Samia
Katika kuadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, jana tarehe 27 Januari 2025, watumishi wa ofisi za VETA Makao Makuu na VETA Kanda ya Kati, wameungana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule na watumishi wa taasisi zingine za Serikali na makundi mbalimbali kupanda miti katika eneo la viwanja vya Nanenane, Nzuguni, Jijini Dodoma, ambapo jumla ya miti 1,480 ilipandwa.
Katika hafla hiyo, Mhe. Senyamule aliipongeza VETA kwa mwitikio mkubwa wa watumishi kushiriki katika zoezi hilo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyoambatana na ukataji keki pamoja na shampeni, Mhe. Senyamule amemtaja Mhe. Dkt Samia kama muasisi wa kampeni ya kuijanisha Dodoma.
“Mhe. Dkt. Samia ndiye alianzisha kazi ya kuijanisha Dodoma alipozindua upandaji miti na neno la “Dodoma ya Kijani” lilianza wakati huo akiwa Makamu wa Rais mwaka 2017 pale Mzakwe ambapo alipanda miti. Tangu wakati huo, tuliendelea na kauli mbiu ya Dodoma ya Kijani na yeye akiendeleza dhamira yake ya kuona Dodoma kuwa ya kijani,” amesema.
Aidha, amehimiza kufuatwa kwa sheria zilizowekwa juu ya upandaji miti kwa mtu mmoja mmoja miti mitano na Taasisi miti 20.
Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA. Anthony Kasore pamoja na menejimenti ya VETA, watumishi wa VETA Makao Makuu pamoja, Mkuu wa chuo cha VETA Dodoma na watumishi wa VETA Kanda ya Kati walishiriki zoezi hilo la kupanda miti.