The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
VETA yashauriwa kuongeza nguvu zaidi katika kutoa mafunzo ya wataalamu wa huduma za hotel
Posted on: Sunday, 02 June 2024
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeshauriwa kuongeza nguvu zaidi katika kutoa mafunzo ya wataalamu wa huduma za hotel, kwani uhitaji bado ni mkubwa hapa nchini.
Ushaur huo umetolewa, tarehe 24 Mei,2024 na Naibu Waziri wa Madini, mheshimwa Dkt Steven Lemomo Kiruswa, alipotembelea banda la VETA, katika viwanja vya AICC, Jijini Arusha ambapo Jukwaa la Tatu la Kuwezesha Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini likiendelea.
"Nashauri VETA muongeze nguvu zaidi katika kutoa mafunzo kwa wahudumu wa hoteli, hasa eneo la ukarimu ili kupata vijana wengi wenye weledi na sifa za kuajirika katika hoteli hapa nchini" amesema Dkt Kiruswa.
Ushauri huo umekuja baada ya mwalimu Hainem Muro kutoa maelezo kwa Naibu Waziri juu ya mafunzo ya fani ya Utalii na Huduma za za Hoteli nayotolewa na chuo cha VETA cha Hoteli na Utalii (VHTTI), kilichopo Njiro, Jijini Arusha.