The United Republic of Tanzania
Ministry of Education Science and Technology
Vocational Education and Training Authority
Skilled Labour Force The Future of Tanzania
VETA yatoa mafunzo kwa madereva 47, makondakta 36 wa kampuni ya Blue Coast ya mjini Geita
Posted on: Wednesday, 28 December 2022
Walimu wa Chuo cha VETA cha Mkoa wa Morogoro (VETA Kihonda) wametoa mafunzo kwa madereva 47 na makondakta 36 wa kampuni ya Blue Coast kwa lengo la kuwawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi na weledi ikiwa ni pamoja na kupunguza ajali zinazotokana na makosa ya kibinadamu.
Mafunzo hayo yametolewa mjini Geita tarehe 19 hadi 24 Desemba, 2022.
Mwalimu Kiongozi wa Udereva wa Magari Makubwa na Mabasi wa chuo cha VETA Kihonda, Ndugu William Munuo, amesema madereva na makondakta hao wamejifunza kwa nadharia na vitendo kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo udereva wa kujihami, huduma kwa wateja na huduma ya kwanza.
Kampuni ya Blue Coast iliyopo mjini Geita inamiliki magari makubwa yanayohudumia wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (Geita Gold Mine - GGM).
Mafunzo yaliyotolewa ni mwendelezo na jitihada za Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) katika kuhakikisha kuwa ujuzi unaotolewa unawafikia wahitaji wote popote walipo.